Diamond Platinumz amezima tafsiri hasi iliyokuwa imewekwa na watu mbalimbali kuwa hayuko katika mstari mzuri na Idris ambaye hivi sasa anataraji kupata mtoto na aliyekuwa mpenzi wake, Wema Sepetu.

Hisia hizo zilichochewa zaidi hasa baada ya mama mtoto wa Diamond, Zari kuvaana na mama mtoto mtarajiwa wa Idris, Wema Sepetu katika mitandao ya kijamii.

Leo, ikiwa ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa ya Idris, Diamond amepost picha ya Idris kwenye akaunti yake ya Instagram yenye wafuasi zaidi ya milioni 1.6, na kuwataka watu wamtakie kheri ya kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa.

“Mtoto wa Mzee Sultan Leo Amezaliwa…. now let’s all drop our Wishes Abi! @idrissulta,” aliandika.

Mtoto wa Mzee Sultan Leo Amezaliwa…. now let’s all drop our Wishes Abi! @idrissultan ?

A photo posted by Chibu Dangote (@diamondplatnumz) on

Chadema wadai wako tayari kuchangisha fedha kuilipa TBC irushe Bunge lote 'Live'
Bweni la Shule ya Sekondari ya Lowassa yateketea kwa moto