Ingawa Diamond Platinumz na Nay wa mitego ni maswahiba walioshibana kwenye sanaa, ushwahiba huo umeshindwa kuwaweka kwenye kiota kimoja cha itikadi za kisiasa.

Diamond ambaye ameonekana kukipigia debe Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kupiga shows nyingi kwenye majukwaa ya chama hicho zinazomuingizia mamilioni ya fedha ameshindwa kumshawishi swahiba wake huyo anayeunga mkono Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kuhamia kwenye chama chake.

Diamond alipost Instagram kipande cha video inayomuonesha akitumbuiza wimbo alioshirikishw na Nay wa Mitego, ‘Muziki Gani’ katika tamasha liliyofanyika  visiwani Zanzibar na kuandika ujumbe unaomlenga swahiba wake huyo.

Bado wewe tu @naytrueboy kurudi Nyumbani….kama nayaona vile yale maselfie yetu na Nguo za Kijani??? #AboutYesterday

A video posted by Chibu Dangote..? (@diamondplatnumz) on

Haikuchukua muda, Nay wa Mitego akamjibu kwa posti inayomuonesha akiwa amesimama huku akiangalia picha ya mgombea urais kupitia Chadema, Edward Lowassa. Aliweka msimamo wake kuwa hivi sasa hatafuata mamiolioni ya fedha anayopata Diamond bali anaangalia harakati za nchi kwanza. 

“Nimekataa siendi popote. Wanasema huu ndo muda wa Wasanii kupiga hela ni kweli, ila mi kwangu itakua tofauti kidogo. Mi ni moja kati ya Wasanii wachache wafanya biashara. Ila kwa kipindi iki cha uchaguzi nimeweka pembeni kidogo maswala ya biashara now ni #Harakati huwezi kumnunua mwanaharakati wa kweli coz ata pesa anajua kuitafuta nje ya #Harakati. Uchaguzi ukiisha we leta izo Deal sasa za mamilioni mia tutafanya, ila kwa sasa tunapigania Maslahi ya nchi na kile wanachotaka watanzania Wengi. Naamini #Mabadiliko2015 @edwardlowassa ndo Raisi wetu… Hakuna nyumbani kwengine nishachukua Uraia kabisaa. Tupo tayari kwa #Mabadiliko2015 @diamondplatnumz hujui kusoma, ata picha huoni?! Watanzania wanataka #Mabadiliko2015″  

Ushindi wa Mayweather ‘wamboa’ Manny Pacquiao
CCM Wamsakama Maalim Seif