Diamond Platinumz anaendelea kujipanga kuhakikisha tamasha la Wasafi linaanza kwa kishindo cha tembo cha kuitikisa Afrika, akiliunganisha na wafalme wa ngoma kali.
Wiki hii, Bosi huyo wa WCB aliweka wazi kuwa mfalme wa ngoma kali kutoka Nigeria, Wizkid ni mmoja kati ya wasanii wa Afrika watakaoshiriki kilele cha tamasha hilo kitakachofanyika jijini Dar es Salaam.
Aliweka wazi mpango huo akiambatanisha na habari ya wimbo wake na Wizkid, baada ya kuchokozwa na Ray Vanny kwenye Instagram.
“Hivi nyie mmelogwa, mbona hamtoi ngoma yenu?” aliuliza Ray Vanny kwenye post ya Diamond aliyoweka picha yake ya Wizkid.
“Inakuja, halafu na ye nawaletea #WasafiFestival2018 Dar… takeni kingine,” alijibu Mondi.
Ayodeji Ibrahim Balogun aka Wizkid ni msanii wa Afrika aliyefanikiwa kutikisa ngome za Marekani, akifanya kazi na Chris Brown, Rihanna, Drake na wengine wengi.
Wimbo wake ‘One Dance’ wa mwaka 2016 ulimpigisha hatua kubwa ukishika nafasi ya kwanza kwenye chati kubwa kwenye nchi 15 ikiwa ni pamoja na Marekani, Canada, Uingereza na Australia.
-
Wanafunzi wanaswa na simu kwenye chumba cha mtihani
-
Avamia hospitali na kuua watatu kwa risasi akimlenga mpenzi wake
Wasafi Festival itaanza rasmi Novemba 24 mjini Mtwara, siku ambayo tamasha kongwe na kubwa la muziki ‘Fiesta’ litakuwa likihitimishwa jijini Dar es Salaam.