Mwaka huu unaonekana kuwa mwaka mwingine wa neema zaidi kimuziki kwa Diamond Platinumz anaezidi kutimka mbio za mafanikio kwenye anga za kimataifa.

Mwishoni mwa juma lililopita, Diamond alipokea habari njema baada ya kutangazwa kuwania tuzo za Uganda zinazojulikana kama ‘Uganda Entartainment Awards 2015’, akiwania kipengele cha Best African Act.

Mkali huyo wa ‘Nana’ anawania tuzo hizo na wasanii wakubwa Afrika akiwemo Wizkid, Patoraking na Tiwa Savage. Tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa Septemba 4, 2015, Kampala, Uganda.
Mtoto wa Tandale [Diamond] aliyeyagusa masikio ya wapenda burudani Tanzania na wimbo wake ‘Kamwambie’ miaka kadhaa iliyopita, anatarajia kubeba tuzo zaidi ya sita za kimataifa katika kipindi cha miezi michache ijayo.

Pamoja na tuzo hiyo ya Uganda, Diamond anategemea tuzo tatu za MTV/MAMA 2015 zilizopangwa kutolewa Julai 18, Durban, Afrika Kusini. Anawania tuzo hizo katika vipengele vitatu ambavyo ni Best Male, Best Act na Best Collaboration.
mtv
Mkali hiuyo wa Ngololo ametajwa pia kuwania tuzo za watu waliofanikisha, ‘African Achievers’ Awards zitakazotolewa Julai 25, 2015 na anawania kipengele cha African Artist of The Year.
Orodha bado inaendelea, msanii huyo pia yuko kwenye kinyang’anyiro cha tuzo za Nigeria zinazojulikana kama Nigeria Entertainment Awards (NEA), zitakazotolewa Septemba 6, mwaka huu, jijini New York, Marekani.

Hivyo, Diamond anatarajia kuwa na tuzo sita za kimataifa endapo mambo yataenda vizuri. Hata kama idadi hiyo itapungua, kutajwa mara nyingi kwenye tuzo kubwa za kimataifa kunamuongezea heshima kubwa katika kiwanda cha muziki Afrika na kuonesha jinsi ambavyo kazi zake zinakubalika.

Watanzania wanahimizwa kumpigia kura na kumsapoti zaidi katika kila tuzo anayotajwa. Kumbuka katika tuzo za MTV/MAMA 2015 Diamond na Vanessa ndio wasanii wanaoiwakilisha Tanzania. Wapigie kura mara nyingi uwezavyo kupitia tovuti ya MTV.

Rapa Wa Afrika Kusini Ampiga Shabiki Jukwaani
Jerry Slaa Autosa Udiwani, Ausaka Ubunge Wa Ukonga