Mwaka umeanza na kasi ya tuzo kwa baba Tiffah, Diamond Platinumz baada ya kutajwa kuwania tuzo za Moreklue All Africa Awards (MAYA 2016) zinazotarajiwa kutolewa jijini Lagos Nigeri, Januari 31.

Diamond ametajwa katika kipengele cha African Music Act ambapo atachuana na wasanii wengine wakubwa barani Afrika akiwemo Wizkid, Davido, AKA, Fuse ODG, Cassper Nyovest na Olamide.

Hii ni tuzo ya kwanza kwa Diamond kutajwa mwaka huu akiwa na historia ya kubeba tuzo nyingi kubwa za Afrika mwaka jana, zikiwemo tuzo tatu za Afrimma, Channel O na nyingine nyingi.

Oscar: Sina Mikwaruzano Na Diego Costa
Walioishi kwa kula nyasi na Udongo Wapewa Msaada