Msanii maarufu wa muziki wa Bongo fleva nchini, Diamond Platnumz amethibitisha tetesi zilizokuwa zikisambaa mtandaoni kuwa amemnunulia nyumba mama mtoto wake Hamisa Mobetto.
Hayo yamethibitishwa leo kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram mara baada ya Diamond kumuhoji mwanae Dylan kuhusu nyumba mpya aliyohamia hivi karibuni ambayo anaishi Hamissa na watoto wake wawili.
Ambapo nyumba hiyo waliohamia hivi karibuni inasemekana kununuliwa na Diamond Platinumz, ni nyumba ya Ghorofa iliyopo maeneo ya Mbezi Beach, Bahari Beach.
Diamond amethibitisha tetesi hizo mapema leo hii baada ya kuandika katika ukurasa wa Instagram wa mtoto wake Dylan akimhoji mwanae kuwa anatumaini ameyapenda makazi yake mapya na Hamisa kujibu kwa kumshukuru kwa nyumba hiyo na anamuomba Mungu aendelee kumshushia baraka Diamond Platinumz kwani wameipenda nyumba hiyo.
”Hope you like the house Daddy” ameandika Diamond.
”We love it… thank you so much May God keep on blessing Abundantly’; amejibu Hamisa
Aidha hii sio mara ya kwanza kwa Diamond kununua Nyumba kwa ajili ya wanafamilia wake kama kwani ameshawahi kumnunulia nyumba mama yake mzazi pia ameshawahi kumnunulia nyumba mzazi mwenzake Zari nchini Afrika Kusini hivyo hii inaonesha jinsi ambavyo msanii huyu anajali maisha bora kwa watu wake wa karibu kwa kuwanunulia majumba ya kifahari ili waweze kuishi mahali pazuri kama yalivyo matamanio ya kila mtu.