Mwanamuziki wa Nassib Abdul maarufu kama Diamond Platnumz amekosolewa mitandaoni kwa kutumia bendera yenye utata katika video ya wimbo wake mpya wa Gidi.
Bendera hiyo ya kundi la Shirikisho la majimbo ya kusini ya Marekani ambayo yalipigania kudumisha utumwa wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe na bendera hiyo inaonekana kama ishara ya mivutano ya ubaguzi wa rangi nchini Marekani.
inasemekana Bendera hiyo kwa sasa huendelea kutumiwa na Wamarekani ambao bado wana Dhana ya ubaguzi na wale weusi ambao wanapinga ubaguzi hawawezi kuisogelea Bendera hiyo popote ilipoperushwa.
Moja ya kipande cha video katika wimbo wa Gidi kina bendera mbili zilizoonyeshwa wakati akicheza huku akiwa na muonekano wa Cowboy.
Maoni ya wadau wa muziki Mtandaoni yanasema mwanamuziki hiyo akae tayari kuhojiwa na Serikali ya Marekani juu ya matumizi ya Bendera hiyo katika muziki wake ingawa anaweza kufungiwa kufanya matamasha nchini humo pia.
Hata hivyo bado msanii huyo wala uongozi wake haujatoka hadharani kusemea jambo hilo.