Diamond Platinumz ana ndoto nyingine kubwa nje ya tasnia ya muziki ambayo ni kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Wasanii inayoshikiliwa hivi sasa na Nape Nnauye.

Mwimbaji huyo amekiambia kipindi cha Papaso cha TBC FM kuwa bado hajajua ni lini ataingia kwenye siasa lakini kama ataacha muziki angependa kushika nafasi hiyo ya juu wizarani.

“Kwa sasa hivi siasa bado ila nikiingia kwenye siasa baadaye akimaliza mheshimiwa Nape nachukua mimi kile cheo cha Waziri wa Michezo,” alisema baba Tiffah.

“Kile nakiweza kabisa kwa sababu mimi ukinimbia sijui kuhusu mpira, movie mimi naweza kabisa nikiwa Waziri, nikavifanya na vikawa na maendeleo. Ni kitu ambacho naweza siyo nasema nataka kuwa mbunge ila mimi nataka ile siku nimeacha kufanya muziki naingia kwenye siasa basi nakuwa Waziri wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na kuboresha vitu,” aliongeza.

 

Picha: Jennifer Lopez aonesha sehemu za siri bahati mbaya akiwa jukwaani
Katibu Tawala wa Katavi afyekwa na kasi ya Magufuli, Baadhi ya Mabalozi warudishwa nyumbani