Diamond Platinumz amefunguka kuhusu barua ya kisheria iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionesha kuwa imetoka kwa mwanasheria wa mpenzi wa zamani wa Zari, Ivan na ndugu yake King Lawrence.

Diamond ameeleza kuwa yeye na Zari hawajawahi kupokea barua hiyo kama ilivyodaiwa na kwamba hiyo ni mbinu ya Ivan kutaka kujipatia umaarufu.

“Unajua lazima tujue kila mtu anatumia mitandao kwa njia zake. Wengine wanatumia kutafutia umaarufu kama hivyo which is not bad, but kupata umaarufu ni kazi sio.. Mtu anatafuta njia yoyote kutafuta umaarufu na watu wakamsikiliza na kupata pongezi kwa sababu amekaa amebuni kitu mpaka watu wakamsikiliza,” Diamond ameiambia XXL ya Clouds Fm.

Diamond alikanusha taarifa za kuwepo mume wa Zari akidai kuwa mrembo huyo toka Uganda hajawahi kuolewa.

Wikendi iliyopita, ilisambaa barua ya kisheria inayoeleza kuwa mtoto aliyejifungua Zari sio mtoto wa Diamond na kwamba baba yake mzazi ni aliyekuwa mpenzi wa zamani wa mrembo huyo, Ivan.

Barua hiyo iliyoonekana kuandikwa na mwanasheria kutoka ‘Web Advocates & Solicitors’ ikienda kwa  Zarina Hassan, ikimtaka kuhakikisha anafanya vipimo vya vina saba (DNA) ili kutambua baba mzazi wa mtoto Tiffah. barua hiyo ilieleza kuwa mteja wa mwanasheria huyo anaamini kuwa Tiffah ni mwanae na sio mtoto wa Diamond kama inavyoaminika.

 

Mancini Aeleza Kwa Nini Amemuacha Kovacic Mateo
Chelsea Waongeza Nguvu Safu Ya Ulinzi