Jalada la Kesi ya madai ya matunzo ya mtoto, Prince Abdul lililofunguliwa na mwanamitindo Hamisa Mobeto dhidi ya msanii Nasseb Abdul maarufu kama Diamond Platinumz limefungwa rasmi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu upande wa watoto.
Leo Februari 13, 2018, baada ya kutoka mahakamani, Diamond amesema walifika kwa ajili ya kuweka kumbukumbu sawa upande wa ustawi wa jamii na mahakama.
Hivyo Diamond na Hamissa Mobeto wameshauriwa kuweka majivuno pembeni ikifika swala la mtoto wao ili waone ni namna gani wanamtengenezea mazigira mtoto wao hasa katika swala zima la malezi.
Wakili wa Mobeto, Walter Godluck amesema ustawi wa jamii unasaidia katika suluhisho la kesi za watoto zinazohusu malezi ambapo baba na mama hukubaliana ni jinsi gani wanaweza kukubaliana kulea mtoto wao.
Hata hivyo mama na baba Abdul pamoja wamekubaliana kumlea mtoto huyo.
Mobeto alifungua kesi hiyo mahakamani akidai matunzo ya mtoto aliyozaa na msanii Diamond ambapo aliomba Mahakama imuamuru Diamond Platinumz kutoa matunzo ya mtoto huyo kila mwezi ya shilingi milioni 5.
Kupitia hati hiyo Mobeto anaomba mahakama imuamuru Dioamnd amuombe msamaha kwa kumsababishia madhara yaliyoishtua familia yake.
Diaomd alipinga madai ya matunzo ya mtoto wao Abdul, akidai kuwa pesa hiyo ni kubwa sana.