Wakazi wa Tanga jana walimpa sababu zaidi za kutabasamu, Diamond Platinumz aliyeingia jijini humo kunogesha kampeni za mgombea urais kwa tiketi ya CCM.

Akiwa mkoani humo, baadhi ya wananchi walioliona gari lake walionesha furaha yao iliyopitiliza wakitamani japo kumshika mkongo huku wengine wakisikika wakiuita ‘rais…rais’ jina ambalo wafuasi wa CCM humuita mgombea wao wa urais anapopita.

Wengine waliohutumbuiza katika mkutano huo wa kampeni ni pamoja na Ali Kiba na Yamoto Band. Bila shaka mvuto wa wasanii hao uliwavuta wengi kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea wa CCM, Dk John Magufuli. mkutano ambao unatajwa kuvunja rekodi ya mikutano katika jiji hilo.

Of course, Diamond ni rais wa Wasafi Classic (WFC), na kudhihirisha ukubwa wake, leo amevunja rekodi kwa kuwa msanii wa kwanza Tanzania kufikisha followers milioni 1 kwenye Instagram.

NHIF Yaingia Makubaliano Ya Udhamini Wa Bima VPL
Barakah Da Prince Apewa Shavu Na Rapa Mkubwa Kenya