Staa wa muziki nchini Nasibu Abdul maarufu kama Diamond Platnumz, amesema kuwa ana mpango wa kulipia ‘kodi ya pango’ kwa kaya 500 kutoka mikoa yote Tanzania.

Amesema kuwa anatamani kugusa mikoa yote nchini kwa baadhi ya familia zenye uhitaji mkubwa wa jambo hilo kufuatia familia nyingi kuathirika na janga la Corona.

“Najua katika kipindi hiki cha Corona, mambo mengi hayajakaa sawa, hususani upande wa biashara, nyingi zimeshuka na kupelekea hali ya kifedha kuyumba na mambo kuwa kidogo magumu kwa wengi wetu… na mimi ni miongoni mwa walio ndani ya janga hili” alisema daimond.

Akizungumza Wasafi FM, Diamond amesema msaada huo utaangalia watu wenye uhitaji mkubwa haswa.

”Kule kwetu uswahili kuna watu wanashida, mtu kama analipa kodi yake ya milioni kayataka mwenyewe, kuna vitu vingine tusijiumize, lakini kuna watu kwakweli unakuta kodi yake masikini elfu hamsini lakini maskini elfu hamsini yenyewe haipati ” amesema Diamond.

Aidha, Daimond aliendelea kusema kuwa wamejipanga ili kuhakikisha wanakwepa figisu hivyo watalazimika kutumia serikali za mitaa pamoja na timu yao ambayo itapita mitaani ili kuwafikia walengwa kama wamama wajane, walemavu na wale wote wenye mahitaji kweli kwa kila mkoa.

Mayayi: Young Africans wasisahau mawinga 2020/21
Taifa la tatu kwa kunyonga watu duniani, limefuta adhabu hiyo kwa watoto

Comments

comments