Ikiwa leo ni siku rasmi ya kuanza kampeni za uchaguzi Mkuu ambapo kila mgombea anatarajiwa kuachia makucha yake hadi Oktoba 24, wasanii wa muziki na filamu wameanza kuwanadi kwa vitendo wagombea wanaowaunga mkono.

Mkali wa Bongo Flava, Diamond Platnumz ambaye hivi karibuni alitangaza kupitia mitandao ya kijamii kuwa anamsapoti mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Maguli, ameanza kufanya hivyo kwa vitendo ambapo ameibadili kabisa hit song iliyomtoa kimataifa ‘Number One’ kuwa wimbo unaomsapoti ‘Dk. Magufuli’.

Katika wimbo huo, Diamond anasikika akimsifia Magufuli kwa ujenzi wa barabara na uwanja wa ndege wa kimataifa ambao bado haujakamilika.

Hii ni dalili kuwa msanii huyo mkubwa, licha ya kukosolewa na mashabiki wake wengi hasa wale ambao hawaungi mkono chama alichokichagua, Diamond atakuwa sehemu ya kampeni ya CCM na atafanya shows kadhaa katika majimbo.

Kwa upande wa Wema Sepetu ambaye aliwahi kuwa mchumba wa Diamond, amepewa nafasi kubwa na CCM kuwahamasisha akina mama na vijana kumchagua Magufuli.

Wema ni Mwenyekiti Mwenza wa kampeni maalum ya chama hicho inayomtaka mama amshawishi mwanae kumchagua Magufuli (Mama Ongea na Mwanao). Wawili hawa wataungana kwenye ziara ya Magufuli baada ya kutofautiana kwa muda mrefu.

Ikumbukwe kuwa Diamond alikuwa mmoja kati ya wasanii walioshiriki katika tamasha kubwa la kumtangaza Edward Lowassa alipokuwa akitangaza nia ya kugombea urais kupitia CCM, lililofanyika jijini Arusha miezi kadhaa iliyopita.

Diamond anaungana na wasanii wengine waliotangaza kumsapoti Magufuli akiwemo Mwana FA, Wema Sepetu na wengine.

Lowassa Amtegea Magufuli
Liverpool Yatangaza Vita Dhidi Ya Juventus