Star wa muziki barani Afrika Diamond Platnumz ameonesha kuguswa na ajali za moto zilizotokea kwenye soko kuu la Kariakoo, Dar es salaam pamoja mkoa wa Morogoro

Diamond ametumia ukurasa wake wa instagram kwa kutoa taarifa yakuwa amepokea kwa masikitiko ajali hiyo iliyotokea Morogoro na sokoni Kariakoo

Aidha katika taarifa yake hiyo amesema kuwa kama kijana atashiriki katika hali na mali kurejesha faraja za ndugu waliopatwa na janga hilo

“Nimepokea kwa masikitiko ajali ya moto iliyotokea Morogoro na sokoni Kariakoo,mwenyezi mungu awatie nguvu wafanyabiashara wote pamoja na kila aliyeguswa na ajali hii ya moto,”

“Kama kijana wa kitanzania Niko tayari kushiriki katika hali na mali katika kurejesha faraja za ndugu zetu waliopatwa na tatizo hilo” ameandika Diamond Platnumz

Hasara kwenye ujenzi ni chaguo lako
Elimu bila ujuzi ni mateso