Diamond Platinumz ameweka wazi kuwa anaogopa kushika simu ya mama mtoto wake, Zari ili asiuumize moyo wake.

Mwimbaji huyo anaamini kuwa urembo na umaarufu wa Zari unamfanya kupokea vitu vingi kwenye simu yake ambavyo akiviona vitampa maumivu ya moyo hivyo amechukua uamuzi wa kujitenga na simu yake kwa kuwa anajua mama Tiffah ni binadamu.

Zari na Diamond Simu

 “Hicho ni kitu cha kwanza ambacho siwezi kudiriki kabisa, sidiriki kwasababu namjua ni binadamu , unajua sometimes ukizingatia na yeye ni mtu maarufu so sometimes watu wengine wanakuwa wanamsumbua, anaweza kukutwa na vishawishi sometimes  anaweza akamjibu mtu akaitikia tu poa, kwangu mimi kikanikwaza kwasababu nampenda kwahiyo ikaniumiza, kwahiyo sitaki kabisa kushika simu yake,” alisema.

Alieleza kuwa ingawa hata yeye simu yake haina Password lakini Zari pia amekuwa anakaa nayo mbali ili asiumie kwa sababu zilezile alizozitaja yeye.

“Kwahiyo simshauri mtu kushika simu ya mpenzi wake, cha muhimu tu kuzingatia kama anakupenda anakujali anakuheshimu na umuone na hivyo vitu, lakini kwenye simu yake mwache afanye chochote anachojua yeye” Baba Tiffah alitoa ushauri wake.

Waziri Mkuu Awafuta Kazi Vigogo Bandarini, Ni Baada Ya Kushtukiza Na Kukuta Madudu
“Kufutwa Sherehe za Siku ya Ukimwi Kumetutia hasara”