Diamond Platinumz na Vanessa Mdee wameiwakilisha vizuri Tanzania katika tuzo za AFRIMA 2015, zilizofanyika jana Dallas, Marekani ambapo Diamond alinyakuwa tuzo 3 huku Vanessa akiondoka na tuzo 1.

Diamond ameshinda tuzo 3 ambazo ni ‘Best Dance Video’, ‘Best Male East Africa’ na ‘Artiste of the Year’, tuzo ambazo zitamuongezea ukubwa kwenye ulimwengu wa muziki.

Kwa upande wa Vee Money, ameshinda tuzo ya ‘Best Female East Africa’, hivyo hii imedhihirisha kuwa yeye ni moja kati ya wasanii wa kike wa Afrika Mashariki ambao kazi zao zinaheshimika na kukubalika zaidi hususan Afrika Mashariki.

Diamond-Afrimma

Tuzo hizi nne zitauongezea heshima kubwa muziki wa Tanzania na kuzidi kufungua milango kwa wasanii wengine kuliteka soko la Afrika na dunia kwa ujumla.

Dar24 tunawapa ‘High Five’ wakali hawa wa Bongo Fleva.

 

 

CCM Walia Na Picha Za Mikutano Ya Lowassa
Kuhusu Kuahirishwa Kwa Uchaguzi Wa Ubunge Arusha Mjini Na Mazingira Ya Kifo Cha Mgombea