Msanii wa Bongofleva, Naseeb Abdul maarufu Diamond Platnumz na mzazi mwenzake, Zari The Bosslady ni miongoni mwa mastaa wa Afrika watakaoonekana katika mtandao wa Netflix hivi karibuni.

Netflix tawi la Afrika Kusini limetangaza kuwa mastaa hao wataonekana katika makala (documentary) waliyoipa jina la ‘Young, Famous & African’ itakayoanza kuruka hivi karibuni kupitia mtandaoni.

Zari The Bosslady kutokea Uganda tayari amewataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula, kwa sababu watapata kufahamu mambo mengi kuhusu wao na kuburudika pia.

Diamond atakuwa Mtanzania wa pili kuonekana Netflix baada ya Idris Sultan ambaye Machi 26 mwaka huu alionekana kwenye mtandao huo kupitia filamu iitwayo ‘Slay’ iliyokutanisha mastaa wa Afrika kama Ramsey Nouah, Fabian Adeoye Lojede, Simphiwe Ngema, Amanda Du-Pont n.k.

Mtando wa Netflix ulianzishwa Agosti 29, 1997 huko California nchini Marekani, hadi sasa watu zaidi ya milioni 200 duniani kote wamejisajili (subscribers) kama wateja kwenye mtandao huo.

Kwa mwaka jana pekee walifikia mauzo ya dola 2.7 bilioni, wameajiri wafanyakazi 12, 135.

Netflix inapatikana duniani kote kasoro nchi za Syria, Korea Kaskazini na China, huku wakiwa na matawi katika nchini za Uholanzi, Ufaransa, Brazil, Uingereza, India, Japan na Korea Kusini, Afrika Kusini na Nigeria.

Hamisa, Samatta wateuliwa kuwa mabalozi uhamasishaji kulipa kodi
Kuvaa barakoa amri Hospitali ya Taifa Muhimbili