Msanii wa muziki, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz, ametua Marangu wilayani Moshi mkoa wa Kilimanjaro na kaahidi kupanda mlima Kilimanjaro hadi kilele.

Aidha msanii huyo amesema safari hiyo inayochukua takribani siku tano alitamani kwenda siku moja na kurudi.

Hata hivyo amesema kutokana na ushauri wa Waziri wa Maliasili na Utalii nchini, dkt. Hamis Kigwangalla, mwenyekiti katika kampeni ya ‘kill challenge twenzetu kilele’ alimtaka aambatane na watu wengine 130 watakaopanda mpaka wote wafike sawa.

”Mimi uwezo wa kupanda mlima siku moja ninao kwani ni sawa na show yangu moja narudi nawaacha kina MwanaFA wakijikongoja ” alisema Diamond

Hata hivyo msanii huyo hakusita mkumsifia Dk Kigwangalla kwa ubunifu wake wa kutumia wasanii katika kutangaza utalii wa ndani na vivutio vinavyopatikana hapa nchini kwa kuwa wao wameshakuwa mabalozi wa bidhaa mbalimbali hivyo hilo ni jambo dogo kwao.

Kwa upande wa msanii Mwana FA amesema kuwa pamoja na nchi kujaliwa vitu vizuri amabvyo havilipiwi kwa Mungu ukweli ni kwamba wasanii bado hawajafanya kazi yao ipasavyo.

Antonio Nugaz awafariji mashabiki Yanga
Mtalii afariki parashuti ilopogoma kufunguka akiruka mlima Kilimanjaro