Pamoja na Kikosi cha Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans kuwa na matokeo mazuri yanayoendelea kuwaweka kileleni Mlinda Lango chaguo la kwanza Djigui Diarra amekiri Ligi Kuu Kuu ni ngumu huku akifunguka Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ imempa ubora.

Diarra ametajwa kwenye orodha ya Walinda Lango Bora na Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ akiungana na Mlinda Mlango wa Manchester United, Andre Onana.

Diarra raia wa Mali amesema anapambana kuhakikisha anavunja rekodi yake mwenyewe aliyoiweka msimu uliopita akiibuka Mlinda Lango bora wa mwaka nchini Tanzania, huku akiipa ubingwa timu yake baada ya nyavu zake kutotikiswa mara 17.

“Msimu huu ni mgumu sana. Sina mwanzo mzuri kama msimu uliopita. Hadi sasa kwenye mechi saba nilizokaa langoni nimeruhusu nyavu zangu kutikiswa mara tatu, lakini hilo halinivunji moyo kwani nina imani kubwa na ukuta unaonilinda,” amesema Diarra ambaye ana ‘clean sheet’ nne hadi sasa.

“Nimerudi na nguvu mpya kwa kuamini kuwa kupoteza ‘clean sheet’ ni sehemu ya mchezo. Nitaendelea kujifua na kupunguza makosa kwenye mechi zilizo mbele, nia ni kuisaidia safu yangu ya ulinzi kulinda ushindi tunaoupata.”

Akizungumzia kutajwa kwenye tuzo za ‘CAF’ Diarra amesema sio jambo dogo kwake linamuongezea nguvu za kujiamini na kufanya mambo makubwa zaidi ili kuendelea kujiweka kwenye ushindani na makipa wakubwa.

“Ubora wangu umeonekana uwanjani kutajwa sambamba na makipa wa timu kubwa. Kwangu ni ushindi ligi ina timu 16 mimi peke yangu kwa Tanzania ndiye nimeonekana. Huu ni ushindi mkubwa kwangu,” amesema.

Tayari najiona mshindi, makipa kumi Barani Afrika jina langu lipo sio kitu kidogo. Nimepata nguvu na kupata imani kuwa kila kitu kinawezekana na nitaendelea kuwa bora zaidi ya hapa nilipo sasa kutokana na kuamini kuwa natazamwa na wengi na ubora wangu umnekuwa darasa.”

Almanusura ya wachezaji Simba SC
Malisa ataka usajili wa Vyuo uhakikiwe Mbeya