Mshambliaji wa zamani wa Klabu ya Chelsesa Didier Drogba ametoa kauli nzito juu ya mmiliki wa sasa wa klabu hiyo ya jijini London baada ya juzi usiku kutolewa katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Baada ya kuzungumza na wachezaji mwishoni mwa juma lililopita kwenye kipigo dhidi ya Brighton, mmiliki wa Chelsea, Todd Boehly, ambaye aliichukua klabu hiyo mwaka jana, aliwafuata tena wachezaji baada ya kupigo cha juzi cha mabao 2-0 dhidi ya Real Madrid, yaliyofungwa na Rodrygo.

Na mkongwe huyo wa Blues, Drogba, ambaye alikuwa mchezaji muhimu wakati wa utawala wa Roman Abramovich, ameshusha shutuma nzito kwa timu yake kutokana matokeo ambayo yalimaanisha Chelsea haitacheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

“Naijua klabu hii ina daraja lake tangu enzi za utawala wa Abramovich, lakini leo hii naiona tofauti. Ni ngumu sana kwangu kuona jinsi inavyoingiza  na kutoa watu,” amesema mshambuliaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Ivory Coast.

“Wanatakiwa kurudi katika kanuni na taratibu za klabu. Siitambui tena klabu yangu. Si klabu ile niliyokuwa naitumikia, kuna mmiliki mpya na mtindo mwingine.

“Bila shaka, tungependa kuilinganisha ya sasa na ile iliyokuwa chini ya (Roman) Abramovich, wakati ambao wachezaji wengi walisajiliwa, lakini uamuzi ulikuwa wa busara na umakini.

“Kusajiliwa wachezaji kama Petr Cech, Andriy Shevchenko, Hernan Crespo, Micheal Essien, Didier Drogba, Florent Malouda na wengine. Usajili huu ulifanywa kwa sababu ya kutwaa mataji.

Robertinho: Tupo tayari kuivaa Wydad AC
Serikali yaomba muda suala la ATCL