Kocha Mkuu wa Simba SC Didier Gomes alitua nchini na kuanza kazi, Januari 24 na leo Mei 04 rasmi anakuwa ametimiza siku 100 kamili tangu awe na kikosi hicho cha Wekundu wa Msimbazi, huku rekodi zake zikimbeba.

Mfaransa huyo bado ni “UNBEATEN” akiwa hajapoteza mchezo wowote katika VPL hadi sasa, pia ameweka rekodi ya Simba kuwa timu pekee kutoka Tanzania kumaliza Kinara wa Kundi A Ligi ya Mabingwa na Bado Gomes ana nafasi ya Kubeba vikombe vitatu msimu huu (VPL, FA na CAFCL).

KWANI GOMES MWENYEWE ANASEMAJE

 “Jambo ninalojivunia ni kukutana na wachezaji wenye uelewa hapa Simba. Kama binadamu kuna makosa ambayo huyafanya lakini kwa kiasi kikubwa hufanya vizuri ndio maana mpaka wakati huu nimepata mafanikio hayo na nina imani nitakuwa na mafanikio mengine zaidi,” anasema Gomes na kuongezea

 “Najisikia vizuri kuwa Simba, ni timu iliyokamilika kuanzia uongozi, benchi la ufundi, wachezaji na hata mashabiki jambo ambalo ni gumu kulipata kwenye timu nyingi za ukanda huu wa Afrika.

 “Siri kubwa ya mafanikio haya ni umoja, ubora na kujitoa kwaajili ya timu, kila mtu wa Simba anatimiza majukumu yake kwa mapenzi makubwa ya klabu ndiyo maana tunafanikiwa na naamini tutaendelea kufanikiwa zaidi ya hapa.”

Inaelezwa kuwa Simba hii ya Gomes ni tishio kuliko Simba nyingine zote zilizopita

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Mei 5, 2021
TAKUKURU: Asukile ameingia mitini