Mashambuliaji Diego Costa ameandika barua ya wazi kwenye mtandao wa kijamii yenye lengo la kuwashukuru mashabiki wa Chelsea baada ya kukamilisha dili lake la kurudi klabu yake ya zamani ya Atletico Madrid.

Costa alijiunga na Chelsea mwaka 2014 akitokea Atletico Madrid jana alikamilisha dili la kurudi Atletico ambayo ataanza kuitumikia rasmi Januari mosi mwakani baada ya adhabu ya klabu yake hiyo mpya kumalizika.

Costa ambaye alikua jukwaani akishuhudia mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya kati ya Atletico Madrid na Chelsea usiku wa kuamkia leo, amewashukuru mashabiki wa The Blues kwa upendo waliomuonesha huku kukiwa hakuna sehemu yoyote ambayo amemtaja Meneja Antonio Conte wala benchi la ufundi la klabu ya Chelsea.

Costa aliandika hivi kwenye Facebook: Maisha mengine huanza wakati mengine yakiwa yanaisha. Maisha yangu ndani ya Chelsea yalianza miaka mitatu iliyopita – miaka mitatu bora kwenye Nyanja zote – na sitaweza kuyasahau.

“Mataji mawili ya Ligi, Ngao ya Jamii, mechi 120, magoli 59 na pasi 24 za magoli na ndio maisha yangu yakaishia hapo, sio kama nilivyotarajia lakini ni njia nzuri.

“Mashabiki bora wa klabu na wachezaji wenzangu pamoja na madaktari na viongozi watabaki milele kwenye moyo wangu na nitaendelea kuwa upande wao pia, na naamini wataelewa sababu ya maisha yangu kwenye klabu kuisha – kwasababu sikuwahi kukata tamaa. Asante Chelsea kwa kila kitu!”

Uganda yapiga marufuku ‘Bunge Live’
Uongozi mpya TFF watembelea SBL