Chama cha soka nchini England FA, kimetangaza adhabu kwa mshambuli wa klabu bingwa nchini humo Chelsea, Diego da Silva Costa baada ya kukamilisha utaratibu wa shitaka walilomfungulia usiku wa kuamkia jana.

Costa, amefungiwa michezo mitatu kutokana na kosa utovu wa nidhamu aliouonyesha wakati wa mchezo wa ligi ya nchini England uliochezwa mwishoni mwa juma lililopita, kwenye uwanja wa Stamford Bridge kati ya Chelsea dhidi ya Arsenal.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26, alifanya tukio la kumpiga mara tatu beki wa Arsenal Laurent Koscielny, na muamuzi Mike Dean aliyechezesha mchezo huo uliomalizika kwa Chelsea kupata ushindi wa mabao mawili kwa sifuri hakuona kilichofanywa na Costa.

FA walimtaka Costa kuwasilisha utetezi wa mashtaka aliyofunguliwa kabla ya saa 12 jana jioni, na mshambuliaji huyo alifanya hivyo lakini alikana kuhusika na tukio la kumpiga Laurent Koscielny, katika dakika 43 ya mchezo.

Kwa mantiki ya adhabu iliyomuangukia Costa, inadhihirisha atakosa mchezo wa hii leo wa michuano ya kombe la ligi (Capital One Cup) dhidi ya Walsall na kisha michezo ya ligi kuu dhidi ya Newcastle pamoja na Southampton.

Gabriel Paulista Yupo Huru Kucheza
Hawa Ndio Wana Hip Hop Walioingiza Fedha Nyingi Zaidi Mwaka Huu ‘Cash Kings’