Mshambuliaji kutoka nchini Hispania, Diego Costa amekanusha kuwasilisha maombi ya kutaka kuondoka Stamford Bridge kama ilivyoripotiwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari mwishoni mwa mwezi uliopita.

Costa aliripotiwa kuwasilisha ombi la kutaka auzwe na kurejeshwa nchini Hispania katika klabu ya Atletico Madrid ambayo alikua akiitumikia kabla ya kusajiliwa na The Blues misimu miwili iliyopita.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27, amesema hakuwahi kufanya maamuzi ya kuomba kuondoka klabuni hapo, na alipoziona taarifa hizo alishangaa.

Amesema anapenda kuendelea kuwepo magharibi mwa jijini London yalipo makao makuu ya klabu ya Chelsea, kutokana na ushindani uliopo kwenye kikosi The Blues ambacho kwa msimu wa 2016-17 kitakua chini ya utawala wa meneja kutoka nchini Italia, Antonio Conte.

Aliposajiliwa klabuni hapo mwaka 2014, Costa alianza vyema na kufanikiwa kumaliza msimu wa 2014-15, kwa kufunga mabao 20 katika michezo 26 aliyocheza.

Alikua sehemu ya wachezaji walioiwezesha Chelsea kutwaa ubingwa katika msimu huo chini ya utawala wa meneja kutoka nchini Ureno Jose Mourinho.

Per Mertesacker: Granit Xhaka Ni Chaguo Sahihi Kwa Arsenal
Inauma: Atumiwa zawadi ya picha za mkewe akifanya ngono kinyume na maumbile, Wasikilize Mke na Mume hapa