Klabu ya Atletico Madrid inaendelea kuushawishi uongozi wa mabingwa wa soka nchini England Chelsea, ili ukubali kumuachia mshambuliaji Diego Costa kabla ya dirisha la usajili halijafungwa usiku wa leo.

Licha ya klabu hiyo kutoruhusiwa kufanya usajili katika kipindi hiki kutokana na adhabu iliyotangazwa na shirikisho la soka duniani FIFA, uongozi wa Atletico Madrid umedhamiria kumrejesha Costa, ili aanze kuwatumikia mwezi Januari mwaka 2018.

Mazungumzo baina ya pande hizo mbili yameripotiwa kuendelea kwa siku ya tatu mfululizo, na baadhi ya vyombo vya habari nchini England vimeripoti kuwa, kuna uwezekano wa biashara ya kuondoka kwa mshambuliaji hiyo ikafanikiwa.

Inasemekana Atletico Madrid wamekubali kumsajili Costa kwa kiasi cha Euro milioni 33, na watampeleka kwa mkopo kwenye klabu za Las Palmas ama Deportivo La Coruna hadi mwezi Januari mwaka 2018, ambapo itakua halali kwao kuanza kumtumia.

Hatua ya Costa kuondoka Chelsea uliibuka baada ya meneja Antonio Conte kumtumia ujumbe mfupi kwa njia ya simu mshambuliaji huyo miezi miwili iliyopita, na kumueleza hamuhitaji tena katika mipango yake ya msimu huu wa 2017/18.

Jux akumbukia mapenzi yake na Vanessa, asema haya kuikaribisha siku yake ya kuzaliwa
Mpinzani wa Kagame apotea, polisi wanawa mikono