Mabosi wa West Ham wana matumaini kwamba hadi kufikia leo Jumatatu (Julai 03) watakuwa wamefikia makubaliano ya namna gani kiasi cha Pauni 105 milioni kitalipwa kama ada ya Uhamisho wa  Declan Rice kutoka kwa wababe waKaskazini mwa jiji la London.

Tayari pande zote zimeshafikia makubaliano ya kuuziana kiungo huyo, lakini kinachosumbua kwa sasa ni jinsi ambavyo kiasi cha pesa ya ada ya uhamisho kitakavyolipwa.

West Ham Utd ilishatoa ruhusa ya Rice kwenda kufanyiwa vipimo vya afya kabla kusaini ya mkataba na mambo yote haya yanatarajiwa kufanyika ndani ya siku mbili hadi tatu zijazo kuanzia leo Jumatatu (Julai 03).

Man City pia ilikuwa sehemu ya timu zilizokuwa kwenye orodha kumsajili ya nyota huyu lakini ilikataa kutoa kiasi cha pesa ambacho West Ham ilikihitaji. Mkataba wa Rice unamalizika mwakani.

Rais Samia atengua, ateua Wakuu wa Wilaya
Rodolfo Borrell abwaga manyanga Man City