Mpango wa Klabu ya Chelsea kutaka kubadilishana mchezaji na pesa na Klabu ya Juventus katika dirisha hili umegonga mwamba baada ya Juve kuhitaji zaidi ya Pauni 35 milioni na Romelu Lukaku ili kumtoa Dusan Vlahovic kwa matajiri hao wa Jiji la London.
Matumaini ya Chelsea hapo awali yalikuwa ni kumtoa Lukaku na kiasi kidogo cha pesa ambacho hakitazidi Pauni 20 milioni ili impate Vlahovic anayeonekana kuwa ni pendekezo la Kocha Maurico Pochetino.
Chelsea bado inatafuta Mshambuliaji, lakini kwanza inapambana kumuondoa Lukaku kikosini ili kupata pesa na nafasi ya kusajili staa mwingine kwani ikisajili kabla ya Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji hajaondoka gharama za mshahara zitakuwa kubwa na Pochettino ameshaweka wazi kwamba hana mpango wa kumtumia katika msimu ujao wa Ligi Kuu England.
Juma lililopita Mkurugenzi wa michezo wa Juventus alifunga safari hadi England kwa ajili ya kufanya mazungumzo zaidi na Chelsea juu ya dili hilo, lakini hakukuwa na mwafaka uliofikiwa kwa aslimia mia.
Dili hilo linaonakena kuwa gumu kukamilika kutokaa kila timu kubaki na msino wake.