Kiungo wa zamani wa Simba SC, Hassan Dilunga amesema msimu ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara yupo tayari kucheza timu yoyote lakini kipaumbele chake cha kwanza ni maslahi.

Dilunga amekuwa nje kwa muda mrefu kutokana na kuumia wakati akiitumikia Simba SC.

Mchezaji huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar na JKT Tanzania amesema; “Nipo tayari kucheza popote kikubwa maslahi, atakaekuja vizuri na tukaelewana nae ndiko nitakapocheza.”

Kuhusu kurudi Simba SC amesema; “Naendelea kuwasikilizia nafanya nao tu mazoezi kama ambayo ninavyofanya na Mtibwa na timu zingine.”

Hata hivyo Mchezaji huyo ameushukuru uongozi wa Simba SC kwa kumtibu kwa ufasaha kipindi alichokuwa akiumwa.

“Nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipowashukuru viongozi wa Simba wamenipambania kuhakikisha napata tiba sahihi, nimepata nawashukuru nimepona kwa asilimia 100,” amesema Dilunga

Kikwete atembelea ubalozi wa Tanzania Korea Kusini
Madaktari wachunguza ugonjwa usiojulikana uliouwa nane