Msanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongofleva), Omary Nyembo maarufu Ommydimpoz amesaini mkataba wa kufanya kazi na kampuni ya Sony Music Entertainment ya nchini Afrika Kusini.

Kupitia ukurusa wake wa Instagram Ommy ameandika “NINAYO FURAHA KUJIUNGA NA MY NEW FAMILY( fanilia yangu mpya) @sonymusicafrica I can’t wait for my New Album to Drop Early Next Year. Dude letu la kwanza kutoka kwenye Album #DEDE tunaliachia leo (jana), Saa 10 jioni…”

Alipoulizwa kuhusu jinsi anavyojisikia mara baada ya kupata ‘donge nono’hilo Dimpoz amesema “Nimefurahi kujiunga na Sony nyumba ya wasanii wenye vipaji duniani, ushirikiano huu ni hatua muhimu sana kwenye muziki wangu na umekuja wakati sahihi kwenye maisha yangu”.

Ingawa taarifa hiyo haijaeleza ni kwa muda gani mkataba huo unadumu Mkurugenzi Mtendaji wa Sony Music Entertainment Africa Sean Watson amesema “Tumefurahia kuunganisha nguvu na Msanii kama Ommy Dimpoz kuufikisha muziki wake kwa Mashabiki wengi iwezekanavyo”

Mapema wiki hii Dimpoz alionyesha kipande cha ngoma yake mpya akiwa na Dj Tira, Dladla na Prince Bulo na kusema analiachia lote Desemba 10 ikiwa ndiyo itakua ngoma yake ya kwanza kuiachia chini ya mkataba na Sony Music.

Mwigizaji Tommy afariki
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Desemba 11, 2020