Aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Habari Young Africans Dismas Ten, ameipongeza Simba SC kwa kutwaa taji la Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara ya nne mfululizo.
Dismas ambaye alichukua nafasi ya kuiongoza Idara ya Habari Young Africans baada ya kuondoka kwa Jerry Murro, ametoa pongezi hizo kwa kuandika ujumbe katika ukurasa wake wa Faceboook.
Dismas ameandika: “Hongera SIMBA kwa kutwaa ubingwa mara NNE mfululizo hii ina maana kwamba timu zingine zina jambo la ziada la kufanya ili kuzuia utawala huu ambao simba imeujenga!!
“Yote kwa yote hili ni soka hii ni ligi na Bingwa ni mmoja Hongereni Mabingwa Simba SC.”
Simba SC leo Jumapili (Julai 18) imekabidhiwa Kombe la Ubingwa Tanzania Bara, baada ya mchezo dhidi Namungo FC Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es salaam.
Katika mchezo huo Simba SC imeshinda mabao 4-0 na kufikisha alama 83.