Aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya Young Africans Dismas Ten ameseama endapo klabu hiyo inajiandaa kumsajili Joash Onyango, itakua na malengo ya kuishia Mzunguuko wa Kwanza Ligi ya Mabingwa Barani Afrika msimu ujao.
Mapema leo Alhamis (April 14) Young Africans ilianza kuhusishwa na taarifa z kumuwania Beki huyo kutoka nchini Kenya, kufuatia mkataba wake na Simba SC kutarajia kufikia kikomo mwishoni mwa msimu huu.
Dismas amesema Young Africans kama kuna ukweli wa taarifa za Young Africans kumsajili Onyango, itakua imefanya makosa makubwa kutokana na umr wa Beki huyo ambaye kwa sasa anaitumikia Simba SC.
Amesema Onyango ni mchezaji mwenye uzoefu wa kucheza michezo ya Kimataifa na amefanya hivyo mara kadhaa akiwa na klabu ya Gor Mahia ya nchini kwao Kenya na Simba SC ya Tanzania, lakini kwa Young Africans sio mahala sahihi kwake, kutokana na umri wake, hivyo ni bora viongozi wakaangalia uwezekano wa kusajili wachezaji wenye umri mdogo.
“Endapo yanga itamsajili Onyango basi itakuwa inajiandaa kuishia raundi ya kwanza ya ligi ya mabingwa msimu ujao!!”
Hata hivyo pamoja na taarifa hizo kushamiri katika mitandao ya Kijamii, Uongozi wa Young Africans haijasema lolote kuhusu mpango huo wa kumsajili Joash Onyango.
Hata hivyo pamoja na taarifa hizo kushamiri katika mitandao ya Kijamii, Uongozi wa Young Africans haijasema lolote kuhusu mpango huo wa kumsajili Joash Onyango.