Mbunge wa Viti maalum anayewakilisha vijana, Mariam Ditopile amekabidhi vitendea kazi zikiwemo Kompyuta zenye thamani ya Shil. Milioni mbili pamoja na fedha taslimu shilingi Laki Sita kwa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Dar Es Salaam.

Ditopile amekabidhi vitu hivyo wakati wa ufunguzi wa Baraza la Vijana ambapo pia amewaasa UVCCM kujitokeza hadharani kujibu tuhuma ambazo zimekua zikielekezwa kwa Chama na Serikali.

Amewataka vijana wa CCM kueneza mazuri ambayo yamekua yakifanywa na Serikali ya Rais Magufuli bila kuona aibu na kuwasihi kusimamia mstari katika kuijenga Tanzania ya viwanda kwa vitendo na siyo maneno.

” Niwasihi vijana wenzangu kuwa mstari wa mbele kuyasema na kuyatangaza hadharani yale yote yanayofanywa na serikali ya CCM katika kutekeleza ilani yake ya mwaka 2015 ambao ndio msaafu unaotuongoza ndani ya miaka hii mitano,”amesema Ditopile

Aidha, amewapongeza UVCCM Dar Es Salaam kwa kuwa waasisi wa kijana na kuongeza kuwa hivi sasa nchi nzima kampeni hiyo imekua kubwa na imezidi kukiimarisha Chama hicho kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

” Nawapongeza kwa kuwa waasisi wa kampeni ya Kijani ambayo imefanikiwa, ila niwanasihi juhudi hizi kubwa zisiishie kwenye matamasha tu bali ni lazima ziwe chachu ya kuhakikisha ushindi mnono kwa Chama chetu katika chaguzi zilizo mbele yetu,” amesema Ditopile.

Afya ya Mugabe yazua gumzo, Rais wa Zimbabwe anena
Bernard Membe ajilipua, 'Haki lazima itendeke hapa'