Baada ya Mshambuliaji wa Young Africans, Ditram Nchimbi kushambuliwa na mashabiki kutumia nguvu nyingi kupambana, lakini umaliziaji wake ni bure, amepata mtetezi anayeamini kinachomponza kuwa ni aina ya mazoezi anayopewa kabla ya mechi na sio tatizo lake.

Nchimbi hajafunga bao lolote kwa zaidi ya mwaka mmoja Ligi Kuu na kuzua mijadala na kejeli kutoka kwa mashabiki, lakini staa wa zamani wa Simba na Taifa Stars, Emmanuel Gabriel amemkingia kifua akisema ni mchezaji mzuri isipokuwa anatakiwa kupewa mazoezi ya kufunga zaidi mazoezini kuliko kukimbia na kutumia nguvu nyingi ambazo akifika ndani ya 18 anakabwa.

“Siongelei kishabiki, nazungumzia kiufundi, nimecheza ndio maana naona uchungu kila ninapoona anapambana sana, lakini bado anashambuliwa, nini kipo nyuma ya mazoezi yake kabla ya mechi, je anapewa yale ya kufunga zaidi ili kumjengea kujiamini?” alihoji Gabriel

Katika hatua nyingine Gabriel amelishauri benchi la ufundi la Young Africans kumbadilishia mazoezi mshambuliaji huyo wa zamani wa klabu za Polisi Tanzania, Azam FC na Njombe Mji FC, ambayo yatamsaidia kumrejesha kwenye mstari wakupachika mabao kama zamani.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Aprili 20, 2021
Mbio za ufungaji bora VPL, Kagere amtaja Dube