Diwani mteule wa kata ya Kinuni iliyopo Zanzibar, Suleiman Mohamed Hassan amefariki dunia juzi Novemba 9 baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 28.

Akithibitisha kutokea kwa kifo hichoKatibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi wa CCM, Catherine Peter amesema kuwa diwani huyo alifariki ghafla baada ya kuanguka nyumbani kwake na kupelekwa Hospitali ya Altabib ambako alifariki dunia muda mfupi baada ya kufikishwa hospitalini hapo.

“Sisi kama CCM tumepokea kwa masikitiko taarifa ya msiba wa diwani Hassan Mohamed na tunaiomba familia yake kuwa na moyo wa subira,” alisema peter.

Msiba huu wa diwani Hassan Mohamed unawaunganisha wanachi wa kata ya Kinuni na wenzao wa kata nyingine tatu wanaosubiri Tume yaTaifa ya uchaguzi kutangaza tarehe mpya ya uchaguzi mdogo ili kujaz nafasi zilizoachwa wazi.

Manara awatuliza mashabiki Simba SC
Taifa Stars yaondoka Uturuki