Diwani wa Kata ya Namawala wilayani Kilombero, Godfrey Lwema (CHADEMA) ameuawa kwa kukatwakatwa kwa mapanga na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake.
Taarifa za awali zimesema kuwa umeme ulikatika katika nyumba yake, hivyo akatoka nje kutizama kama kuna shoti maana nyumba za jirani zilikuwa na umeme, ndipo alipokutana na kundi la wenye mapanga na kuanza kumkatakata hadi kupoteza uhai wake.
Aidha, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei amethibitisha kuuawa kwa diwani wa Chadema Kata ya Namwawala, Jimbo la Mlimba, na kusema kuwa kwasasa hawezi kuzungumza chochote kwasababu hajajua sababu za mauaji hayo.
“Mauaji yametokea usiku huu na polisi wameshafika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu, sasa hivi tuko kwenye uchunguzi na tunaomba wananchi watusaidie kutoa taarifa za watu wanaodhani kuwa wanahusika kwenye tukio hili na tutahakikisha tunawapata,” amesema Kamanda Matei.
Hata hivyo, kwa upande wake mbunge wa Jimbo la Kilombero, Peter Lijualikali alithibitisha mauaji hayo na kudai kuwa yatakuwa yamepangwa.
-
Video: Dkt Tulia azungumzia tetesi za kugombea ubunge Mbeya, ‘Ni haki yangu’
-
Video: Rais Magufuli asafiri nje ya nchi kushiriki mkutano wa wakuu wa nchi EAC
-
Video: Tunashirikiana vizuri na wapinzani Ubungo- DC Kisare