DJ Arch Jnr, mtoto mwenye umri wa miaka mitatu tu ameweza kuonesha ujuzi wake wa kucheza na mashine na kuchanganya miziki, hatimaye kuibuka mshindi wa shindano la Afrika Kusini linalofahamika kama ‘SA Got Talent’.

Kutokana na ushindi huo, DJ Arch Jnr ameweza kujizolea kiasi cha fedha zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 74 za Tanzania.

Mtoto huyo ameweka rekodi ya kuwa mshindi mwenye umri mdogo zaidi katika historia ya mashindano hayo. Ujuzi alionao kulinganisha na umri wake ulimfanya ajizolee sifa za kutosha kwa mashabiki wa shindano hilo waliomshangilia muda wote.

DJ Arch Jnr, alianza kuoenesha ujuzi wake kwa umma tangu akiwa na umri wa miaka miwili tu ambapo baba yake aliamua kumtengeneza kuwa ‘brand’ kwa kuweka video za kazi zake kwenye YouTube.

Hata hivyo, baba yake huyo aliyemfundisha, alisema kuwa mwanae bado ana mambo mengi ya kujifunza kwenye tasnia hiyo ili awe DJ mzuri zaidi kadri anavyokuwa . Alisema kwa sasa mwanae anahitaji kuwa na laptop iliyofanyiwa ‘set up’ sambamba na mashine maalum ya DJ kwa ajili ya kumkumbusha muda wa kuanza show.

Hata hivyo, wapo walioanza kueleza kuwa huenda baba yake amekuwa akimuandalia mixing na kisha kuziweka kwenye mashine hiyo, kitu ambacho baba yake amekikanusha vikali kupitia ukurasa wake wa facebook. Alisema kila alichofanya kwenye show ni uhalisia kama ilivyokuwa ikionekana.

 

 

Ban Ki-Moon Ampongeza Rais Magufuli
Manny Pacquiao Asimamisha Shughuli Za Pambano