Mabingwa wa soka nchini England, Chelsea wapo katika hatua za mwisho kumsajili beki kutoka nchini Senegal na klabu ya Nantes ya nchini Ufaransa Papy Djilobodji kwa ada ya uhamisho wa paund million 4.

Djilobodji anatarajiwa kuwasili jijini London hii leo na kufanyiwa vipimo vya afya kabla ya kukamilisha mpango wa kujiunga na klabu hiyo ambayo imeanza vibaya msimu wa ligi kwa kufungwa michezo miwili, kushinda mmoja na kutoka sare mmoja.

Meneja wa Chelsea Jose Mourinho, anatarajiwa kuwa na beki huyo mwenye umri wa miaka 26, ili kufanikisha mipango ya kuisuka safu ya ulinzi klabuni hapo ambayo imeonyesha kuwa na ubutu tangu mwanzoni mwa msimu.

Maamuzi ya kusajili wa beki huyo wa Senegal pia yamechagizwa na kukwama kwa usajili wa beki wa kati wa klabu ya Everton, John Stones ambaye alihitajika kwa udi na uvumba huko magharibi kwa jijini London.

Djilobodji, bado ana mkataba wa mwaka mmoja na klabu ya Nantes, na huenda akasajiliwa moja kwa moja na klabu ya Chelsea mwishoni mwa msimu huu, kama atafanya vizuri kwenye kikosi cha The Blues.

Undani Wa Dk. Slaa Kuimwaga Chadema, Lowassa Na Kustaafu Siasa
Makamba Ashangazwa Na Vichwa Vya Habari Kuhusu Lowassa