Mchezaji anayeorodheshwa katika nafasi ya kwanza katika mchezo wa Tenis duniani Novack Djokovic amepuuzili mbali madai ya udanganyifu katika ngazi za juu za mchezo huo.

Djokovic amesema kuwa udanganyifu wa mechi hauwezekani katika tenisi ya ngazi ya juu huku madai ya ufisadi yakizonga kuanza kwa michuano ya Australia Open.

Mchezaji huyo ambaye amekiri kukataa pauni laki moja na kumi elfu ili kushindwa katika mechi alipoanza mchezo huo, amesema hatahivyo hakuna ushahidi wa udanganyifu miongoni mwa wachezaji wa ngazi za juu.

”Ni uvumi tu”,alisema raia huyo wa Serbia ambaye ameshinda mataji 10 ya Grand Slam.

BBC na BuzzFeed imepokea nakala za siri ambazo zina ushahidi wa udanganyifu katika mchezo huo.

Nakala hizo zinaonyesha katika muongo mmoja uliopita,wachezaji 16 ambao wameorodheshwa katika 50 bora duniani wamepelekwa katika kituo cha maadili cha mchezo huo kwa shauku kwamba huenda walikubali kushindwa baadhi ya mechi.

Wachezaji wote wakiwemo washindi wa Grand Slam waliruhusiwa kuendelea kushindana.

Chris Kermode, Mkuu wa muungano wa wachezaji tenisi wa kulipwa amekana madai kwamba ushaihidi wa udanganyifu katika mchezo huo umefichwa kwa sababu fulani ama unaweza uanchunguzwa zaidi.

Lakini aliongezea”Huku ripoti za BBC na BuzzFeed ikitaja matokeo kuanzia 10 iliopita,tutachunguza habari zozote mpya”.

Waziri wa serikali ya Uingereza John Whittingdale ameiambia BBC kwamba mchezo wa tenisi unafaa kujifunzo kutokana na makosa ya michezo mingine na kuchukua hatua za haraka.

Lowassa asema wabunge, mameya wazembe kufukuzwa Chadema
Cannavaro: Sijachukizwa Na Maamuzi Ya Mkwasa