Mcheza Tennis kutoka nchini Serbia, Novak Djokovic amesonga mbele katika michuano ya Wimbledon Championships (Wimbledon Open) baada ya kumgaragaza mpinzani wake kutoka nchini Serbia, Marin Cilic.

Mchezo kati ya wawili hao uliochukua muda wa saa moja na dakika 49, ulishuhudia Djokovic anayeshika namba moja kwa ubora dunia upande wa wanaume akichanua kwa ushindi wa seti tatu kwa sifuri ambazo ni 6-4, 6-4 na 6-4.

Ushindi huo unampeleka Djokovic katika hatua ya nusu fainali ambapo atapambana na mshiriki kutoka nchini Ufaransa, Richard Gasquet ambaye amefanikiwa kumshinda Stan Wawrinka kutoka nchini Uswiz kwa seti tatu kwa mbili ambazo ni 4-6, 6-4, 6-3, 4-6 na 9-11.

Mchezo mwingine wa hatua ya robo fainali upande wa wanaume ulishuhudia Gilles Simon kutoka nchini Ufaransa akipambana na Rodger Federer ambaye aliibuka kidedea kwa ushindi wa seti tatu kwa sifuri ambazo ni 3-6, 5-7 na 2-6.
Naye Vasek Pospisil, kutoka nchini Canada alipapatuana na Andy Murray kutoka nchini Scotland ambaye aliishinda kwa tatu kwa sifuri ambazo ni 4-6, 5-7 na 4-6.

Kutokana na matokeo hayo, sasa Andy Murray kutoka nchini Scotland atapambana na Rodger Federer katika mchezo wa hatua ya nusu fainali.

Leo, michuano hiyo inaendelea kwa michezo ya hatua ya nusu fainali upande wa wanawake ambapo, Serena Williams kutoka Marekani atapambana na Maria Sharapova kutoka Urusi huku mwanadada Garbiñe Muguruza kutoka Hispania akionyeshana ubabe na Agnieszka Radwańska kutoka Poland.

Hummels: Bado Nipo-Nipo Sana BVB
Nicki Minaj Ampa Sharti Meek Mill Ili Amzalie Mtoto