Kocha Msaidizi wa Young Africans Cedrick Kaze amesema wapo tayari kwa ajili ya mchezo Mzunguuko wa 17 wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Geita Gold utakaopigwa leo Jumapili (Machi 06).
Young Africans ya Dar es salaam itakua mgeni katika mchezo huo utakaounguruma kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza majira ya saa kumi jioni.
Kaze amesema wanahitaji alama tatu za mchezo huo licha ya kutarajia kuwakosa baadhi ya wachezaji wao kutokana na sababu mbalimbali.
Wachezaji ambao hawatakua sehemu ya kikosi cha Young Africans dhidi ya Geita Gold FC ni Ni Jesus Moloko, Djuma Shaban pamoja na Khalid Aucho ambao hawa hawapo fiti.
Aucho inaripotiwa kwamba amepata majeraha huku Djuma akitajwa kuwa na Malaria na Moloko yeye ni majeruhi na alifanyiwa upasuaji hivi karibuni.
Pia yupo Yacouba Songne ambaye huyu ameanza program maalumu pamoja na Abdalah Sahibu, ‘Ninja’ beki ambaye ametumia dakika 2 uwanjani ilikuwa mbele ya Kagera Sugar kutokana na kutokuwa fiti.
“Tunajua kwamba mchezo utakuwa mgumu lakini tupo tayari ili kuweza kupata matokeo, mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi tunaamini kwamba tutashinda,”
“Baadhi ya wachezaji wetu hawatakua nasi, lakini tunaamini tuna kikosi kipana ambacho kinamuwezesha mchezo yoyote aliye FIT kucheza na kutimiza lengo la kupondoka na furaha ya ushindi.” Amesema Kocha Kaze.
Young Africans inaongoza msimamo wa Ligi Kuu Tanzanai Bara ikiwa na alama 42, baada ya kucheza michezo 16, huku Geita Gold FC iliyong’ara katika michezo kadhaa iliyopita ikiwa alama 21 zinazoiweka katika nafasi ya 07 kwenye msimamo.