Beki wa Pembeni wa klabu ya Young Africans Djuma Shaban amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu jukumu la kupiga mikwaju ya Penati ya klabu hiyo inayoongoza msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa tofauti ya alama 11.

Djuma Shaban alipiga mkwaju wa Penati dhidi ya Azam FC na kuifungia Young Africans bao la kusawazisha kipindi cha kwanza, baada ya Saido Ntibazonkiza kushikwa miguu na Mlinda Lango Ahmed Salula.

Beki huyo aliyesajiliwa Young Africans akitokea AS Vita Club ya DR Congo mwanzoni mwa msimu huu, amesema jukumu la kupiga Penati linamuhusu baada ya kukabidhiwa na Benchi la Ufundi chini ya Kocha Nabi.

Amesema jukumu hili ni kawaida kwake, kwani alipoklua AS Vitas Club aliwahi kuwa mpiga Penati zote zilizokua zikitokea ndani ya dakika 90, na alifanya vizuri mara zote.

“Suala la kupiga Penati sijaanza Young Africans ni jukumu maalum nililopewa tangu nikiwa AS Vita, hivyo nilikuwa nalifanyia mazoezi kabisa na sasa nimelizoea sikumbuki nilikosa lini mara nyingi nimekuwa nikipata,”

“Penati haina mwenyewe ni kujiamini na kupiga ukiwa na akili kwamba timu nzima wewe ndio umeibeba ukikosa umewaangusha wachezaji na benchi la ufundi.” amesema Djuma

Djuma ameshaifungia Young Africans mabao matatu msimu huu, mawili yakiwa ya Penati alizopiga dhidi ya Ruvu Shooting na Azam FC na moja dhidi ya KMC FC.

Dkt.Biteko atatua mgogoro wa Wachimbaji wa Dhahabu Chamwino
Harsi Said: Tutachukua Ligi Kuu, ASFC