Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla amekana kuwa na uhusiano wowote wa kirafiki au uadui na Tatibu Juma Mwaka, maarufu kama Dk. Mwaka akidai sio rafiki wala adui yake.

Dk. Kigwangalla ameandika ujumbe kwa umma kuhusu uamuzi wake wa hivi karibuni wa kumfuatilia tabibu huyo na kuamuru akamatwe na jeshi la polisi kwa kile alichoeleza kukiuka taratibu za kitabibu na tiba mbadala.

Naibu waziri huyo amekanusha taarifa zilizoandikwa na gazeti moja kuwa aliwahi kusoma shule moja na tabibu hiyo mkoani Kigoma na kwamba waliwahi kuwa marafiki hata katika ngazi za familia kabla ya urafiki wao kuingia dosari kwa sababu binafsi na kugeuka maadui.

Tabibu Juma Mwaka

Tabibu Juma Mwaka

“Muulizeni Ndg. Juma Mwaka anaposema ana ugomvi ‘binafsi’ na mimi, anamaanisha nini, ugomvi upi? Juu ya nini? Awape taarifa kamili. Mimi Sina ugomvi naye. Kwanza sikuwahi kumjua kabla ya ziara yangu ya kikazi pale Foreplan, ntakuwaje na ugomvi na mtu nisiyemjua? Si utakuwa ujuha huo?” Dk. Kingwangalla alihoji.

Alisema kuwa tabibu Mwaka amekuwa akikiuka taratibu na sheria za tiba mbadala. Alisema Disemba mwaka jana aliliagiza Baraza la Tiba Mbadala kuwaita matabibu wote na kuwaelekeza kufuata sheria lakini tabibu huyo aliendelea kutotii alichoelekezwa.

“Kufanya haya ni kuvunja sheria za nchi. Na makosa haya yana adhabu zake. Sisi kama Serikali tumeagiza hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake,” alisema.

Dk. Kigwangalla ambaye hivi karibuni alitoa saa 24 kwa Jeshi la Polisi kumkamata tabibu Mwaka, alisema kuwa licha ya kutofanikiwa kwa muda Serikali itamtia nguvuni na atachukuliwa hatua kisheria kwani ina mkono mrefu.

 

Mourinho Ajipa Matumaini Makubwa Kwa Pogba
Lema apaza sauti yake kwa Rais Magufuli, amchongea Ole Sendeka