Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi na makamu wake wa kwanza, Maalim Seif Sharif Hamad leo Januari 14, 2021 wataanza ziara ya siku mbili wilayani Chato Mkoni Geita.

Dkt. Mwinyi ametua katika uwanja wa ndege wa Geita-Chato na kupokelewa na waziri wa Nishati,  Dkt. Merdad Kalemani na Waziri wa Uvuvi, Mashimba Ndaki.

Naye maakmu wa kwanza wa Rais Maalim Seif, amewasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza na kupokelewa na ujumbe wa viongozi wa Mkoa wa Geita.

Akiwa Chato Dk  Mwinyi na ujumbe wake watakuwa na mazungumzo na mwenyeji wao, Rais John Magufuli.

Mara baada ya mazungumzo hayo Dkt. Mwinyi  na Maalim Seif watatembelea soko la kimataifa la dagaa la Kasenda na kuzungumza na wananchi na wafanyabiashara wa soko hilo.

Gwajima ashangazwa na uongo, ufichaji dawa
Jafo aagiza Mkurugenzi kusimamishwa kazi