Dkt Luis Shika ambaye amerejea nchini na mabilioni ya fedha pamoja na vipande kadhaa vya dhahabu amefunguka juu ya malengo yake ya kufanya uwekezaji nchini ambapo amesema anampango wa kufungua viwanda tofauti tofauti 30.
Shika amezungumza hayo pindi alipohojiwa na moja ya chombo cha habari hapa nchini na kusema kuwa anataka kuwaonyesha wote waliodhani utajiri wake ni wauongo na ambao bado hawaamini juu Ya umiliki wa fedha nyingi alizonazo.
Hivyo sasa amekuja na kauli mbiu yake inayosema ”Tutaelewana Tu” akilenga wale wote wasio na imani juu ya utajiri wake na kudai huu ni wakati wa kuonyeshana makali.
Ametaja maeneo tofauti ambayo anatarajia kufanya uwekazaji na kufungua viwanda, ametaja kufungua kiwanda cha Mafuta, madini, muziki, chakula na vingine ambavyo bado hajaviweka wazi, amesema katika muziki tayari ameshaanza kumuongoza moja ya msanii hapa nchini ambapo alikuwa nae pindi akifanya mahojiano haya.
-
Video: Nape akubali lawama ya ‘Bao la mkono’, JPM awapasha viongozi wa dini
-
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Juni 13, 2018
”Uwekezaji mkubwa nitakaoufanya naingiza viwanda thelathini hii ni pamoja na musical industry kama tulivyoanza pamoja na msanii wangu, itakuwa pamoja na Food indusrty Petroleum na Mining” Amesema Shika.
Dkt Shika aliyepata umaarufu katika mnada wa nyumba za Lugumi na neno lake 900 itapendeza mara baada ya kubuluzwa mahakamani kwa kosa la kuvuruga mnada huo kwa kuahidi kiasi cha pesa na kushindwa kulipia asilimia 25 ya fedha hizo alizotaja akidai kuwa fedha zake zipo Urusi na zikirejea atafanya malipo hayo.
Aidha siku chache zilizopita Dk. Shika alitangaza kurejea nchini na fedha hizo na kuonyesha baadhi ya nyaraka za umiliki wa fedha hizo na vipande kadhaa vya dhahabu.