Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Wilbroad Slaa ameelekea nchini Marekani kwa ajili ya mapunziko akiwa na familia yake.

Akiongea katika mahojiano na Tido Mhando wa Azam TV, mahojiano yaliyorushwa leo asubuhi na kituo hicho cha runinga, Dk Slaa ameeleza kuwa hivi sasa nyumba yake iko chini ya ulinzi wa Usalama wa Taifa kutokana na vitisho anavyopokea.

“Ninatishiwa maisha, ni lazima nichukue tahadhari. Ninatishiwa kupigwa mawe, ni kweli nalindwa na usalama,” alisema.

Dk Slaa ambaye alitangaza kustaafu siasa za vyama, alisema kuwa anashangaa kusikia watu wanaulizi kuhusu yeye kuishi katika hotel ya Serena wakati hata mwaka 2010 alikuwa akiishi katika hotel hiyo na watu hawakumuuliza.

Mbali na kupumzika, Dk Slaa anatarajia kujiendeleza na Kozi fupi ya Sheria na Lugha akiwa nchini Marekani.

Duru zinaeleza kuwa Dk Slaa aliondoka nchini jana jioni kuelekea Marekani.

 

Boateng: De Bruyne Hawezi Kuikomboa Man City
Kipyenga Cha Ligi Kuu Kupulizwa J.Mosi