Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) leo anatarajiwa kuweka hadharani mustakabali wake kisiasa, jijini Dar es Salaam.

Taarifa zinaeleza kuwa Katibu Mkuu huyo alijiweka kando na harakati za kampeni mara tu baada ya chama chake kumkaribisha Edward Lowassa na kumpa nafasi ya kugombea urais akiwakilisha vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), anatarajiwa kuzungumza na waandishi wa habari majira ya saa saba mchama jijini Dar es Salaam na kuweka wazi uamuzi wake.

Dk. Slaa ambaye aliwahi kutoa kitabu cha ‘List of Shame’ ambacho kilimtaja Edward Lowassa kuwa kati ya mafisadi wakubwa nchini akisisitiza kuwa na ushahidi wa kutosha, anatarajiwa kutoa kauli ambayo itabadilisha kabisa hali ya kampeni za urais zinazoendelea nchini kutokana na ushawishi wake mkumbwa.

Awali, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe aliwaambiwa wafuasi wa chama hicho kuwa Dk. Slaa alionesha kutoridhishwa na uamuzi uliochukuliwa na chama hicho hivyo wakamuomba apumzike kwanza aache safari iendelee, atajiunga na safari hiyo atakapoamua tena.

Sitta Adai Wanaweza Kumshtaki Lowassa, Lowassa Awataka Wananchi Wasiogope
Magufuli: Tanzania Haihitaji Vyama Vya Siasa