Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi, ameyaagiza mashirikisho na vyama vya michezo nchini ambavyo vinasimamia Timu za Taifa kuwasilisha ratiba na mikakati ya timu hizo kwa mwaka 2021 kufikia mwisioni mwa mwezi huu.

Dkt. Abbasi ameyasema hayo jana Jumatatu Desemba 07, jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua na kisha kutoa mada kwenye semina ya maafisa habari na wasemaji wa vyama, mashirikisho na vilabu mbalimbali vya michezo kuhusu namna ya kusemea na kutangaza masuala ya michezo iliyoandaliwa na Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya Kampasi ya Dar es Salaam.

“Tumebaini moja ya sababu inayokwamisha Timu zetu za Taifa kufanya vizuri Kimataifa ni pamoja na baadhi ya Vyama na Mashirikisho yanayosimamia timu hizo kwa niaba ya wananchi kuzichukulia timu hizo kama timu zao binafsi’”

“Wanaposhindwa kufanya maandalizi ya maana tunaanguka kama Taifa. Hii sasa basi. Nataka kufikia Disemba 31 mwaka huu mipango na ratiba zote za Timu za Taifa ziwe zimewasilishwa kwenye Baraza la Michezo la Taifa nao wataileta Serikalini ili tujue mwaka 2021 tunaanzaje,” alisema Dkt. Abbasi.

Serikali kupitia Baraza La Michezo La Taifa (BMT) kila mwaka imekua ikivitaka vyama vya michezo na mashirikisho kuwasilisha mipango kazi ya mwaka mzima.

KMC FC yaisukia mipango Mtibwa Sugar
Mapya yaibuka kesi ya 'Papa Msofe'