Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt.Bashiru Ally ameongoza mamia ya waombolezaji kuaga miili kumi ya wanafunzi waliofariki kwa kuungua na moto ulioteketeza bweni la watoto wa kiume katika shule ya msingi Byamungu Islamic iliyoko wilayani Kyerwa Mkoani Kagera.

Wanafunzi hao walifariki usiku wa kuamkia Septemba 14, ambapo wanafunzi wengine watano walijeruhiwa.

Wanafunzi waliojeruhiwa wanaendelea na matibabu katika hospitali ya rufaa ya Bugando iliyopo jijini Mwanza na mmoja anaendelea kupatiwa matibu katika hospital ya Nyakahanga iliyopo wilayani Karagwe mkoani Kagera.

Belarus yatangaza kufunga mipaka yake
Mgombea ubunge NCCR-Mageuzi atangaza kujitoa

Comments

comments