Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai leo Aprili 1, 2021 amewaapisha Wabunge watatu walioteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wabunge hao ni Balozi Dkt. Bashiru Ally, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk na Balozi Liberata Mulamula ambao kwa pamoja wameapa mbele ya Spika wa Bunge.

Aidha, Spika Ndugai ameahirisha vikao vya Bunge mpaka April 6 mwaka huu saa 3:00 asubuhi, ili kutoa nafasi kwa Mawaziri kufanya makabidhiano na kuwatakia heri ya sikukuu ya Pasaka waumini wote wa madhehebu ya Kikristo.

Uwaziri ni cheo cha muda - Ndugai
Rais Samia apangua Baraza la Mawaziri