Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amefungua mkutano wa mwaka wa kiutendaji wa Maafisa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara za Kisekta, Taasisi za umma pamoja na sekta binafsi zinazotoa huduma za Ustawi wa Jamii nchini na kutoa maelekezo mahsusi yatakayofanya sekta hiyo kuwa imara na kutoa huduma bora katika Taifa.

Akifungua Mkutano huo jijini Dodoma ambao umehudhuriwa na viongozi mbalimbali ikiwemo Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, Dk Biteko ametaka kuhakikishwa kuwa mchakato wa mapitio ya sheria ya mtoto na kanuni zake unakamilika ili kuhakikisha watoto wanapata ulinzi na malezi stahiki.

Pia ameagiza mchakato sheria ya wataalamu wa ustawi wa jamii inakamilika ili kupanua wigo na kusimamia maadili wa utoaji wa huduma za ustawi wa jamii huku Wakurugenzi wa Halmashauri wakitakiwa kutenga fedha kwa ajili ya huduma za Ustawi wa Jamii kwa mujibu wa mwongozo wa mipango, bajeti na taarifa za Ustawi wa Jamii.

Ukatili: Wanawake, Watoto wahanga waku

Makamba ateta na Waziri wa Viwanda UAE
Polisi wa doria wawekwa mtu kati na Walevi